Michezo

Jose Mourinho ajiandaa sasa kurejea uwanjani

July 31st, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

BERLIN, Ujerumani

KOCHA Jose Mourinho amesema yuko karibu kurejea uwanjani mara tu atakapoitwa na timu inayomfaa.

Tangu atimuliwe na Manchester United mwezi Desemba 2018, Mourinho amekuwa akifanya shughuli zake lakini sasa kuna uvumi kwamba huenda akaajiriwa hivi karibuni.

“Nimebakia na muda mfupi wa kufikiria pa kwenda, kutafakari lakini hivi karibuni nitapewa kazi, ingawa kuna marafiki wengi wanaoniambia niendelea kufurahia maisha. Binafsi sipendi kukaa bila timu,” akasema.