Habari

Jowie aachiliwa kwa dhamana ya Sh2 milioni pesa taslimu

February 13th, 2020 1 min read

Na MAUREEN KAKAH

JOSEPH Irungu ‘Jowie’ aliyeshtakiwa katika mauaji ya Monica Kimani ameachiliwa kwa dhamana ya Sh2 milioni pesa taslimu.

Akitoa uamuzi katika Mahakama Kuu Jaji James Wakiaga amemuonya dhidi ya kutoa kauli zozote kuhusu kesi inayomkabili katika vyombo vya habari au katika kurasa za mitandao ya kijamii.

Ametakiwa awe akiripoti kwa chifu wa eneo lake kila Alhamisi ya mwisho kila mwezi ili naye amkabidhi Naibu Msajili kuhusu uzingatiaji wa agizo hilo.

Miongoni mwa masharti mengine, Jowie ametakiwa awasilishe paspoti yake mahakamani na akaonywa dhidi ya kuitafuta nyingine au stakabadhi nyingine ya usafiri wakati wote ambao kesi haijaamuliwa.