Habari Mseto

Joyce Akinyi akamatwa tena kuhusu mihadarati

July 14th, 2019 1 min read

Na Benson Matheka

MFANYABIASHARA mbishi wa Nairobi, Joyce Akinyi na mwanamume raia wa Congo, walikamatwa jana kwa kushukiwa kulangua dawa za kulevya.

Polisi walisema kwamba walivamia chumba ambacho Akinyi na mwanamume huyo walikuwa wakiishi katika mkahawa wake wa Deep West jijini Nairobi na kupata kilo 2 za heroin ya thamani ya Sh3 milioni.

Inasemekana kuwa Akinyi anayekabiliwa na shtaka la kulangua dawa za kulevya katika mahakama ya Kibera alikuwa na paspoti iliyoonyesha ni raia wa Congo.

Wapelelezi wanashuku kwamba alikuwa akitumia paspoti hiyo kuzuru mataifa tofauti nchini kuendeleza biashara ya mihandarati.

Wawili hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga wakisubiri kufunguliwa mashtaka.

Hii ni mara ya tatu kwa Akinyi kukamatwa kwa kushukiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

Mnamo 2015 alikamatwa pamoja na watu wengine watatu na kushtakiwa katika kesi inayoendelea katika mahakama ya Kibera.