Jubilee yapiga kampeni kali za kupangua UDA uchaguzini Rurii

Jubilee yapiga kampeni kali za kupangua UDA uchaguzini Rurii

Na WAIKWA MAINA

KUNDI la wanasiasa wa Jubilee wikendi waliendeleza mpango wa kudhoofisha ushawishi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) katika uchaguzi mdogo wa Wadi ya Rurii, Kaunti ya Nyandarua, unaofanyika Jumanne.

Wanasiasa hao walitumia rasilimali nyingi kulipia matangazo katika runinga na redio mbalimbali kwenye jitihadi za kuvumisha mgombeaji wa Jubilee.

Wakiongozwa na Gavana wa Nyandarua Francis Kimemia, Waziri wa Maji Sicily Kariuk, Gavana wa Laikipia Ndiritu Muriithi, Kiongozi wa Wengi Bungeni Amos Kimunya na Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu, walifanya kila wawezalo kuhujumu kampeni za UDA.

Kikosi cha kumpigia debe mwaniaji wa UDA, Muraya Githaiga, kiliongozwa na Mbunge Mwakilishi wa Nyandarua Faith Gitau, Rigathi Gachagua (Mathira) na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro.

Katika vituo mbalimbali, wanasiasa wa UDA walikumbana na mapokezi mabaya huku wapiga kura wakiwataja kama wasaliti kwa kupinga mswada wa BBI bungeni.

You can share this post!

Celta Vigo yazamisha matumaini finyu ya Barcelona kutawazwa...

Spurs waadhibu Wolves na kujiweka pazuri kufuzu kwa Europa...