Habari Mseto

Jumwa afikishwa mahakamani

August 28th, 2020 1 min read

NA Philip Muyanga

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ameshtakiwa kwa makosa ya ufisadi katika mahakama moja ya Mombasa. Mbunge huyo ambaye alifika mbele ya hakimu mkuu Edna Nyaloti alikana mashtaka hayo..

Aliachiliwa kwa thamana ya Sh5 milioni ama pesa taslimu Sh2 milioni.

Kupitia wakili wake, mbunge huyo alikuwa ameomba kuachiliwa bila dhamana yeyote lakini korti ikakataa.

Upande wa  mashtaka huikukataa kumwachilia kwa dhamana lakini ukasema haifai kuwa chini.

Wenzake waliokuwa wameshtakiwaa pampja waliomba kupunguziwa dhamana na wakapunguziwa kutoka Sh10 milioni hadi Sh2 milioni aau pesa taslimu Sh500,000.

Kesi hio itasikizwa tena Septemba 21.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA