Habari Mseto

Jumwa akamatwe – Haji

August 27th, 2020 1 min read

Mohamed Ahmed and Charles Lwanga

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji ameagiza kukamatwa kwa mbunge wa Malindi Aisha Jumwa kwa utumizi mbaya wa Sh57 milioni kutoka.

Bw Haji pia aliagiza kukamatwa kwa watu wengine saba ambao ni  wanachama wa Malindi NG-CDF.

Maafisa wengine sita wa Malindi NG-CDF tayari wamekamatwa.

Bw Haji alisema kwamba Bi Jumwa na hao saba watatakamwa kwa kuhusika kwa utumizi mbaya wa fedha.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba biashara  mingi zinazomilikiwa na Bi Jumwa zilipokea pesa hizo na kwa njia za udangayiku wakaziweka kwa kampuni binafsi.

Kampuni zilizopewa fedha hizo ni  Multisereve, Kaseru, Bizcot na Gadu.

Bw Haji alisema kwamba baada ya uchunguzi waligundua kwamba Sh19 milioni zililipwa kampuni ya Multiserve.

 

TAFSIRI NA FASUTINE NGILA