Habari Mseto

Jumwa aleta stakabadhi zenye kasoro kortini

October 23rd, 2020 1 min read

BRIAN OCHARO NA FAUSTINE NGILA

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amekana mashtaka ya maujai Alhamisi. Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma aliomba apewe muda ili kutafuta stakabathi za kumnyima thamana.

Korti iliupa upande wa mashtaka saa mbili  kumpa mshatiwa wakili.  Jaji alisema kwamba haitawezekana kufanya uamuzi wa kumpa mbunge huyo dhamana kwani kuna stakabathi anahitaji ili afanye maamuzi hayo.

Mapema leo jaji wa mahakama kuu Njoki Mwangi alilazimika kusitisha  kusikizwa kwa kesi ya Jumwa kujibu mashtaka kwani stakabathi za uchunguzi wa kiakili zilikuwa hazipatikani.

Jaji alikuwa ameomba kupewa stakabathi za  ripoti ya uchunguzi wa kiakili ya Bi Jumwa lakini korti iligundua kwamba ilikuwa na sahihi isiyo ya daktari wa kiakili  ambaye hufanya uchunguzi wa kiakili Mombasa.

Lakini upande wa mashtaka ulieleza kwamba sahihi hiyo ilikuwa imewekwa na dakatari mwingine kwani anayepaswa kuweka sahihi alikuwa tayari ameshastaafu.

Bi Jumwa na mlinzi wake wanashtakiwa kwa mauaji ya Jola Ngumbao aliyekuwa mfuasi wa chama cha ODM kwenye kampeni zilizofanyika wadi ya Ganda.