Habari Mseto

Jumwa na mlinzi wake ni wapenzi – Korti

October 30th, 2020 1 min read

BRIAN OCHARO NA FAUSTINE NGILA

Mbunge wa Malindi  Aisha Jumwa na mlinzi wake  wanaoshatakiwa kwa makosa ya mauaji yaliyotokea 2019 wanaaminika kuwa wapenzi kwa muda wa miaka sita sasa, zilionyesha rekodi za korti.

Ripoti zilionyesha kwamba Bi Jumwa na mlinzi wake Bw Geoffrey Otieno Okuto walikuwa wapenzi huku wakifanya kazi pamoja.

“Ripoti zilisema kwamba Bi Jumwa alitengana na mumewe wa kwanza kwa muda wa zaidi ya miaka 20 iliyopita. Kwa muda wa miaka sita amekuwa kwenye uhusiano na Bw Otieno ambaye wameshtakiwa pamoja,”ilisema ropoi hiyo.

Ripoti zilionyesha pia Bw Otieno ameoa na akona watoto wawili.

Ripoti hizo zilikana madai kwamba Bw Otieno alitengana na mkewe Judith Awinja ambaye walifunga ndoa 2009.

“Mshukiwa annaminika kushungilia maitaji ya familia yake na uhusiano mem ana mkewe amabye anaaminika kuwa hajaajiriwa lakini huunza vifaa vya uembo ili kukidhi maitaji ya familia”..”

Ripoti hiyo iliongeza kwamba mke wa Bw Otieno anafahamu uhusiano wa mumewe na mbunge huyo..