Habari Mseto

Jumwa na Otieno kuchunguzwa akili

October 20th, 2020 1 min read

NA BRIAN OCHARO

Mbunge wa Malindi  Aisha Jumwa na mwenzake  Geoffrey Okuto Otieno watabakia kizuizini hadi Alhamisi ambapo watajibu mashtaka ya mauaji yalioyotokea  2019.

Mahakama kuu ya Mombasa iliagiza Jumatatu kwamba wawili hao wazuiliwe ili wafanyiwe uchunguzi wa kiakili.

Ms Jumwa na  Mr Otieno walifikishwa kortini baada ya mkurugenzi wa mshtaka ya umma Noordin Haji kuthibitisha mashtaka yao ya mauaji ya Bw Gumbao Jola wakati wa uchanguzi mdogo wa wadi ya Ganda.

Jaji Njoki alipeana maaizo hayo baada ya kukataa maombi yay a kuachiliwa kwa dahamana.

“Naagiza kwamba washukiwa hao waendelee kuzuiliwa iliwafanyiwe uchunguzi wa kiakili,”alisema jaji huyo.

Bi Jumwa na Bw Otieno watapelekwa Hospiatli ya Coast General kufanyiwa uchunguzi wa kiakili.

Wawili hao walikuwa wameiomba korti waachiliwe kwa dhamana ya 500,000 ambayo walikuwa wameachiliwa nayo mwaka jana.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA