Juventus pazuri kuipiku PSG, Real kunasa Pogba

Juventus pazuri kuipiku PSG, Real kunasa Pogba

IMEKUSANYWA NA CECIL ODONGO

VIGOGO wa Italia Juventus wamejiweka pazuri kuipiku Real Madrid na PSG ili kutwaa huduma za kiungo wa Manchester United Paul Pogba ambaye kandarasi yake na timu hiyo inatamatika mwishoni mwa mwezi huu wa Mei.

Juventus wako tayari kumpa Pogba, 29, mshahara wa Sh1.1 bilioni kila mwaka ambayo ni Sh23 milioni kila wiki.

Pia Pogba atapokezwa bonasi ya juu na kitita kikubwa kama ada ya usajili.

Huku Paulo Dybala na mkongwe Giorgio Chiellini nao pia wakitarajiwa kuondoka klabuni humo, Juventus imemhakikishia Pogba kuwa yeye ndiye atakuwa mwanasoka anayeenziwa na kutambuliwa zaidi kikosini.

Pogba anatarajiwa atashirikiana na Dusan Vlahovic ambaye pia alijiunga na klabu hiyo mnamo Januari.

Pogba alijiunga na Manchester United kama mchezaji chipukizi mnamo 2012 hadi 2016 ambapo alihama Old Trafford kwa kima cha Sh12 bilioni.

Hata hivyo, mara hii atakuwa akirejea jijini Turin kutoka Man United bila kulipiwa ada zozote.Ingawa alitarajia angejiunga na Real Madrid au PSG, klabu hizo mbili zinaonekana zimeonyesha hazina nia ya kutwaa huduma zake.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wapewa idhini ya kupiga risasi na kuua wahalifu wa...

Nunueni chanjo kutoka Afrika, Ramaphosa ashauri

T L