Juventus wakomoa Zenit na kuingia 16-bora UEFA

Juventus wakomoa Zenit na kuingia 16-bora UEFA

Na MASHIRIKA

JUVENTUS walipepeta Zenit St Petersburg ya Urusi 4-2 mnamo Jumanne usiku jijini Turin, Italia na kufuzu kwa hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Paulo Dybala wa Argentina alipachika wavuni mabao mawili ya Juventus na kuchangia jingine.

Hata hivyo, beki Leonardo Bonucci alijifunga katika dakika ya 26 na kuwarejesha Zenit mchezoni.

Dybala aliyefungua karamu ya mabao katika dakika ya 11, alifanya mambo kuwa 2-1 kupitia penalti ya dakika ya 58 baada ya Federico Chiesa kuchezewa visivyo ndani ya kijisanduku cha Zenit.

Chiesa alifungia Bayern bao la tatu kunako dakika ya 73 kabla ya Alvaro Morata kuzamisha kabisa wageni wao mwishoni mwa kipindi cha pili.

Sardar Azmoun ndiye aliyefunga bao la pili la Zenit sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa.

Ushindi wa Juventus unamaanisha kwamba wanafuzu kwa hatua ya 16-bora kutoka Kundi H baada ya kushinda mechi zote nne kufikia sasa. Wanaongoza kundi kwa alama 12, tatu zaidi kuliko nambari mbili Chelsea.

Zenit wanakamata nafasi ya tatu kwa pointi tatu huku Malmo ya Uswidi wakivuta mkia bila alama yoyote.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Chelsea pua na mdomo kuingia 16-bora UEFA baada ya...

Jinsi ya kuandaa maharagwe

T L