Juventus washuka hadi nafasi ya tisa kwenye Serie A baada ya kupoteza mechi ya nne ligini msimu huu

Juventus washuka hadi nafasi ya tisa kwenye Serie A baada ya kupoteza mechi ya nne ligini msimu huu

Na MASHIRIKA

JUVENTUS walishuka hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya Italia (Serie A) baada ya kupepetwa 2-1 na Verona katika mechi iliyokuwa ya nne mfululizo kwa masogora wa kocha Massimiliano Allegri kupoteza.

Giovanni Simeone alifunga mabao mawili chini ya kipindi cha dakika tatu na kuwapa wenyeji Verona uongozi wa 2-0. Ingawa Weston McKennie alirejesha Juventus mchezoni katika dakika ya 80, Verona walisalia imara na wakadhibiti vilivyo wageni wao.

Matokeo hayo yaliwapaisha Verona hadi nafasi ya nane kwa alama 15 sawa na Fiorentina na Juventus ambao kwa sasa wameachwa na Napoli na AC Milan kwa alama 13.

Juventus walielekeza langoni makombora manne pekee katika muda wote wa dakika 90 japo nusura wafunge bao kupitia Paulo Dybala katika kipindi cha kwanza.

You can share this post!

Crystal Palace waduwaza Man-City kwenye EPL

Muturi yuko ngangari kuwania urais

T L