Kabras, Strathmore na Menengai Oilers wang’aria wenyeji Kenya Cup

Kabras, Strathmore na Menengai Oilers wang’aria wenyeji Kenya Cup

Na GEOFFREY ANENE

KLABU ya Kabras Sugar iliendelea kutetemesha kwenye Ligi Kuu ya raga ya wachezaji 15 kila upande maarufu kama Kenya Cup baada ya kupepeta Top Fry Nakuru 31-3 ugani Nakuru Athletic, Jumamosi.

Ntabeni Dukisa aliweka wanasukari hao kutoka kaunti ya Kakamega kifua mbele 7-0 alipoongeza mkwaju wa mguso wake mapema katika mchuano huo.

Vijana wa kocha raia wa Afrika Kusini Jerome Muller walienda mapumzikoni wakiwa 12-0 juu baada ya nahodha Daniel Sikuta kufuma mguso wa pili.

Mguso wa Keith Imbwaga na mkwaju kutoka kwa Dukisa uliweka Kabras 19-0 mbele kabla ya Nakuru kupunguza mwanya huo kupitia penalti.

Hata hivyo, Kabras ilijibu na miguso kutoka kwa Teddy Akala na Hillary Mwanjilwa naye Dukisa akahitimisha na mkwaju.

Kabras, ambayo ilishinda Kenya Cup msimu 2015-2016 na kufika fainali msimu 2016-2017, 2017-2018, 2018-2019 na 2021, ilijibwaga uwanjani dhidi ya Nakuru baada ya kukung’uta Blak Blad ya Chuo Kikuu cha Kenyatta 49-3 Novemba 27.

Katika michuano mingine iliyochezwa Desemba 4, Mwamba ilitupa uongozi mwembamba wa alama 13-12 ikichabangwa na wageni wao Strathmore Leos 38-18 ugani Impala Club jijini Nairobi.

Mechi ya pili ugani humo ilishuhudia vijana wa kocha Gibson Weru, Menengai Oilers wakicharaza wenyeji Impala Saracens 28-10.

You can share this post!

Kocha wa Senegal amtaka Klopp aheshimu AFCON

Shujaa yapigwa na Great Britain kumaliza raga ya Dubai 7s...

T L