Kafyu yasitishwa Marsabit, Kerio kuwezesha kura

Kafyu yasitishwa Marsabit, Kerio kuwezesha kura

JACOB WALTER Na FRED KIBOR

SERIKALI imesitisha kwa siku tatu utekelezaji kafyu katika maeneo yanayokumbwa na utovu wa usalama kaunti za Marsabit na Elgeyo Marakwet.

Kulingana na kamishna wa Marsabit, Paul Rotich, kusitishwa huko kutafanyika kati ya jana Jumatatu na kesho Jumatano ili kuruhusu wakazi kushiriki uchaguzi.

Katika Bonde la Kerio, Kamishna wa eneo hilo Maalim Mohamed alisema kafyu italegezwa.

“Tutalegeza kafyu inayoendelea kwa angalau siku tatu lakini doria za polisi zitaimarishwa,” alisema.

Bw Maalim alisema kando na kuwatuma maafisa zaidi eneo hilo, nambari maalum ya simu yenye vituo 24 katika kaunti zote 14 za Bonde la Ufa imebuniwa ili kusimamia masuala ibuka.

Maeneo yaliyoathiriwa na amri ya kafyu katika Elgeyo Marakwet ni wadi yote ya Tot yenye kata nane, sita katika wadi ya Chesongoch na kata za Kapyego, Chesuman na Arror.

You can share this post!

TAHARIRI: Kususia kura si jibu la kupata uongozi bora

Ruto apiga kura katika kituo cha Kosachei

T L