Michezo

Kahaba ataka Giggs amvishe pete kisha wazidi kujaza dunia

July 28th, 2019 2 min read

NA MASHIRIKA

MWEZI mmoja baada ya aliyekuwa mke wa Ryan Giggs, Stacey Cooke, 40, kutwaliwa na mwanamuziki Max George, 30, kahaba Thomas Imogen, 36, naye amemtaka mwanasoka huyu wa zamani wa Manchester United kumvisha pete ya uchumba.

Giggs mwenye umri wa miaka 45 aliwahi kudumu na Stacey katika ndoa kwa kipindi cha miaka 10 kabla ya wawili hao kutemana rasmi mwishoni mwa 2017. Talaka hiyo ilimvunia Stacey kima cha Sh6.5 bilioni.

Mapema Juni, Stacey alionekana na Max kwa mara ya kwanza katika ufuo wa Ibiza huku wakiponda raha katika mkahawa wa kifahari uliokuwa ukiwatoza Sh150,000 kwa usiku mmoja.

Max anaanza kulimenya tunda la Stacey ambaye ni mama wa watoto wawili miezi mitano baada ya kutemwa na mwigizaji maarufu Michelle Keegan, 32.

Stacey alikatiza uhusiano wake na Giggs baada ya jicho la nje la sogora huyo kumwelekeza kwa wahudumu wa kike wa mabaa na kahaba Imogen ambaye kwa sasa analiwania upya penzi hilo.

Giggs aliwahi pia kuburudishwa kimapenzi na Natasha ambaye ni mke wa kakaye Rhodri. Uhusiano huo wa siri ulidumu kwa kipindi cha miaka minane. Imogen ana watoto wawili – Siena na Siera ambao aliwapata katika uhusiano wake wa awali na mwigizaji Adam Horsley.

Mwishoni mwa mwaka jana, Imogen alifanyiwa upasuaji ili kufanya matiti yake yasimame tisti kifuani kama ya kibinti kibichi.

Katika mahojiano yake na gazeti la The Sun, alidokeza kwamba uzazi ni kiini cha kuanguka kwa maziwa yake na hiyo ndiyo iliyokuwa njia ya pekee ya kuyarejesha kwenye mvuto wa zamani.

Alisema lengo lake ni kurejesha usichana ambao utamfanya kuwa kivutio kwa Giggs na wanasoka wengine maarufu ambao siku zote wamekuwa wakilihemea buyu lake la asali.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Giggs alimwajiri hawara Kate Greville kuwa Afisa wa Mawasiliano wa GG Hospitality ili ashirikiane na Imogen kuwatia kishawishini wanaume wenye kuwataka kimapenzi katika hoteli hiyo ya vyumba 133.

Hoteli ya GG Hospitality iliyofungwa majuzi, ilisifika kwa biashara ya ukahaba hasa kwa wanasoka wenye kiu ya kuzima uchu wao kwa huduma za ngono ya haraka jijini Manchester. Hoteli hiyo iliyoko karibu na uwanja wa Old Trafford inamilikiwa na Giggs na sogora wa zamani wa Man-Utd, Gary Neville.