Dondoo

Kalameni akataa kuhudhuria sherehe ya rafiki yake aliyemwalika dakika za mwisho

Na JANET KAVUNGA August 28th, 2024 1 min read

KOMBANI, KWALE

KALAMENI wa hapa alikataa kuhudhuria sherehe ya kulipa mahari ya rafiki yake alipomwalika dakika za mwisho.

Jamaa alimlaumu rafiki yake kwa kutomhusisha katika maandalizi ya sherehe hiyo hadi dakika za mwisho alipomwalika.

“Umekuwa ukiandaa sherehe hii kwa mwaka mmoja na ulialika watu katika kamati ya maandalizi. Ningekuwa rafiki yako wa dhati unavyodai, ungeniweka msitari wa mbele katika maandalizi na sio kunialika dakika za mwisho. Hii inamaanisha kwamba haunithamini na nimekuwa nikijidanganya kuwa wewe ni rafiki yangu,” jamaa alisema na kukataa katakata kuhudhuria shereh hiyo.

Inasemekana mwenye sherehe hakuweza kumshawishi jamaa kubadilisha nia.