Kimataifa

Kamala Harris aendea kura za Waamerika kwa Waarabu

Na MASHIRIKA August 29th, 2024 2 min read

WASHINGTON, AMERIKA

WAKILI mwenye mizizi yake Misri ambaye alikuwa afisa wa Idara ya Usalama nchini Amerika Brenda Abdelall, amejiunga na kampeni ya urais ya Kamala Harris, ili kusaidia kutafuta kura za wapiga kura wa Waamerika wenye asili ya kiarabu katika baadhi ya majimbo ambayo yanaweza kusaidia kuamua matokeo ya uchaguzi wa Novemba 5, 2024.

Waamerika wenye asili ya kiarabu wana ushawishi mkubwa katika baadhi ya majimbo yenye ushindani mkali.

Abdelall atakuwa na jukumu la kuimarisha uungwaji mkono kutoka kwa jamii hiyo ambayo ilikasirishwa na Amerika kwa kutoa msaada wa kivita kwa Israeli huko Gaza.

Makamu wa Rais wa Amerika Kamala Harris, tayari amemwajiri wakili mwingine mwenye asili ya Kiafghanistani Nasrina Bargzie, ili kufikia jamii ya Waislamu.

Kwenye kinyang’anyiro hicho, Bi Harris yuko bega kwa bega na mgombea urais wa Republican Donald Trump.

Makamu huyo wa Rais Amerika anawania kiti hicho cha hadhi ya juu kupitia Democratic Party.

Kura kutoka kwa Waamerika ambao ni Waislamu zina uwezo mkubwa kusaidia kuamua matokeo katika majimbo yenye ushindani kama vile Michigan, ambalo limekumbwa na maandamano kuhusu vita vya Israeli katika Gaza.

Rais wa Amerika Joe Biden, alipata sehemu kubwa ya kura kutoka kwa Waarabu na Waislamu mwaka 2020, lakini msaada wake kwa Israeli uliochangia idadi kubwa ya vifo huko Gaza, ulikasirisha wengi katika jamii hiyo.

Jamii hiyo ilizindua kampeni ya kutokuwa na imani dhidi yake kwenye uteuzi wa mgombeaji wa Democratic.

Wiki ijayo, Harris anatarajiwa kufanya kampeni yake katika Jimbo la Michigan, eneo linaloaminika kuwa na idadi kubwa ya Waislamu na Waarabu nchini humo.

Wapiga kura zaidi ya 100,000 walipiga kura dhidi ya Bw Biden, ambaye alijiondoa kama mgombea urais Julai 21, 2024.

Baadhi ya wanaharakati wanasema kuwa Bi Harris anawajibika kwa sera na utawala wa Biden kuhusu Israeli na vita vya Gaza.

Wiki jana, katika mkutano wa chama cha Democratic, wanaharakati wanaounga Palestina, walisema Harris alishindwa kujitenga na hali hiyo.

Wanaharakati hao ambao pia hawalengi kumpigia kura Bw Trump, walizindua kampeni dhidi ya Harris na kuwaomba wafuasi wao kuwaunga wagombea wa vyama viingine.

Abdelall, ambaye ni mzaliwa wa Ann Arbor, Jimbo la Michigan, alisajiliwa kwenye kampeni ya Harris kutafuta kura za Waarabu Waamerika, aliwahi kuwa mshauri mwandamizi katika Idara ya Usalama nchini humo.

Aliingia katika idara hiyo Januari 2021, muda mfupi baada ya Trump kuondoka madarakani kama mkuu wa wafanyakazi katika Afisi ya Idara ya haki za kiraia