Habari

Kamati ya bunge yafukuza maafisa kwa kukosa taarifa kuhusu KQ kutwaa JKIA

February 26th, 2019 1 min read

Na CHARLES WASONGA

KAMATI ya bunge kuhusu Uchukuzi imewafukuza maafisa kutoka kwa Wizara ya Uchukuzi, mashirika ya Kenya Airways (KQ) na Kenya Airports Authority (KAA) kwa kukosa taarifa ya pendekezo kuhusu mpango wa KQ kutwaa usimamizi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Maafisa wa wizara walioongozwa na katibu Esther Koimmet huku KQ ikiongozwa na mkurugenzi wake Sebastian Mikosz.

KAA ilikuwa inaongozwa na MD Jonny Anderson.

Wabunge pia wamesisitiza kuwa sharti Waziri James Macharia afike katika kikao hicho.

Mwenyekiti wa kamati David Pkosing ameamuru warejee saa sita na dakika 15 (12:30p.m).