Kampuni ya bima, Aga Khan kutoa matibabu ya bure

Kampuni ya bima, Aga Khan kutoa matibabu ya bure

KAMPUNI ya Bima ya Jubilee, Chama cha Akiba na Mikopo cha Solution na Hospitali ya Aga Khan zimeanzisha kambi ya matibabu bila malipo katika kaunti ya Meru kuwahimiza wakazi kubaini hali zao za afya.

Hafla hiyo itakuwa ya siku saba katika matawi ya chama hicho yaliyoko Chuka, Nkubu, Meru, Nanyuki, Timau, na Maua.

Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya bima ya Jubilee Bi Njeri Jomo alisema kwamba zoezi hilo ni njia moja ya kusaidia wakazi kuimarisha hali zao za afya.

“Kwa muda mrefu, watu wamekuwa wakitafuta huduma za afya wakiugua jambo linalotatiza matibabu kwa kuwa ugonjwa unabainika ukiwa umeenea,” alisema Jomo

“Tunataka kupalilia desturi ya watu kupimwa kila wakati ili wakazi waweze kuimarisha hali zao za afya,” alisema Jomo.

  • Tags

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Kocha Paulo Bento ajiuzulu baada...

Serikali kufunga shule za msingi za mabweni

T L