Kampuni ya Crystal River yajizolea sifa kwa kutengeneza bidhaa za urembo na usafi

Kampuni ya Crystal River yajizolea sifa kwa kutengeneza bidhaa za urembo na usafi

Na MAGDALENE WANJA

BI Shirlene Nafula ni mmiliki wa kampuni ya Crystal River ambayo hutengeneza bidhaa za urembo na usafi.

Biashara hii aliianza mnamo mwaka 2014 baada ya kunyimwa visa ya kusafiri na kusomea uzamili katika somo la Biopharmaceuticals katika Chuo Kikuu cha Kings College kilichoko London, Uingereza.

“Nilitarajiwa kuwa na kiwango kikubwa cha pesa za kulipa karo ya kila mwaka na za kukimu mahitaji yangu ya miezi 12 pamoja na malazi katika makao yangu mapya ila sikuwa na hela za kutosha,” akasema Bi Nafula.

Hakujua la kufanya na hivyo aliona ndoto yake ya kusomea kozi aliyotaka ikizama.

Baadhi ya bidhaa za urembo na usafi zinazotengenezwa na kampuni ya Crystal River. PICHA | MAGDALENE WANJA

Tangu utotoni, alikuwa na ndoto ya kufanya biashara katika sekta ya urembo, na hivyo akaamua kufanya utafiti ili kumwezesha kuanza biashara.

“Utafiti wangu ulinielekeza katika sekta ya urembo na bidhaa za kutumika wakati wa kufanya usafi,” anaongeza Bi Nafula.

Baada ya tafiti, alisajili biashara hiyo mnamo Machi 2015.

“Nilikuwa na mtaji wa Sh10,000 ambao nilipewa na marehemu nyanyangu. Mamangu pia alinisaidia katika kununua baadhi ya vyombo vya plastiki na kemikali nilizotumia kutengenezea bidhaa,” akasema Bi Nafula.

Biashara yake imefana kwenye soko la bidhaa za urembo na lile la bidhaa za usafishaji.

Shirlene Nafula ni mmiliki wa kampuni ya Crystal River ambayo hutengeneza bidhaa za urembo na usafi. PICHA | MAGDALENE WANJA

Baadhi ya bidhaa anazouza ni pamoja na Bio Pearl Hand wash and Hand Sanitizer, Bethels Hair shampoo, Shanea body lotion, shower gel, Glycerine na Granmas Multi-Purpose wash.

Bi Nafula ananuia kupanua biashara yake kwa kuongeza bidhaa zaidi.

Bio Pearl Hand wash ni mojawapo ya bidhaa ambazo hutengenezwa na kampuni ya Crystal River. PICHA | MAGDALENE WANJA
  • Tags

You can share this post!

WANTO WARUI: Wizara iangazie zaidi vyuo vya ufundi ili...

Uhaba wa nafasi kulazimu wanafunzi elfu 24 Pwani kusomea...

T L