Kampuni yakanusha madai ya ubaguzi wa rangi kwa waajiriwa

Kampuni yakanusha madai ya ubaguzi wa rangi kwa waajiriwa

NA DAN OGETTA

KAMPUNI moja ya bima nchini imekanusha madai kwamba, baadhi ya maafisa wake wanatumia matamshi ya ubaguzi wa rangi kuwatambua wafanyikazi wa Kenya.

Katika mawasiliano ya barua pepe, mmoja wa mameneja wa kampuni hiyo mwenye asili ya Kihindi aliwarejelea wafanyakazi wa Kenya kama ‘nyani’ wanaostahili kufutwa kazi kwa kile alichotaja kuwa utendajikazi wao duni.

Kampuni ya Kenindia ambayo ilianzishwa nchini 1978 imekuwa ikitoa huduma nchini.

Katika barua pepe, meneja wa fedha Mohan Jha aliandika kuwa wafanyakazi Wakenya wanafaa kufutwa kazi kutokana na utendajikazi wao duni.

“Tunafaa kuwafuta kazi hawa nyani. Hawafanyi kazi vizuri,” akaandika meneja huyo.

Bw Jha alikuwa akijibu Meneja Mkuu wa Mauzo, Kabali Arivalagan, ambaye amekuwa akilalamikia tabia ya dereva wake na kumwomba mkurugenzi mkuu kumbadilishia dereva.

Katika ujumbe wa barua pepe unaorejelewa: Ombi la kumwajiri dereva mpya na kumfuta kazi John Mukirai Karanja kwa sababu ya utovu wa nidhamu kazini, Bw Arivalagan alimlalamikia msimamizi wake Bw Sharmaji.

“Kuanzia leo, simtaki Bw Karanja awe dereva wangu. Nataka nibadilishiwe dereva. Kwa sababu ya masuala ya usalama, nitakuwa nikitumia Uber hadi nitakapobadilishiwa dereva,” akaandika meneja wa fedha.

Inashukiwa mifumo ya kampuni hiyo ilidukuliwa kuingiza madai ya ubaguzi wa rangi.

  • Tags

You can share this post!

ZARAA: Mfumo wa bustani za PVC unaweza kusaidia raia...

Serikali yaonya wasafiri kuhusu magaidi

T L