Kampuni yatengeneza rangi za kisasa

Kampuni yatengeneza rangi za kisasa

Na WANGU KANURI

KUHAKIKISHA kuwa nyumba imedumu na inawalinda kiafya wanaoishi pale imekuwa changamoto kwa Wakenya wengi.

Hii ni kwa sababu, nyingi ya nyumba hizo hupata nyufa kwenye kuta, zinaota kungu, zina miundo hafifu ya saruji, zinachambuka rangi na huwa na unyevunyevu haswa baada ya kulowa maji.

Wenye nyumba hizo hulazimika kukarabati nyumba zao mara kwa mara huku, huku ikiwagharimu pesa nyingi huku wakazi wakilalamikia kutatizika kiafya haswa kutokana na kupumua ule unyevunyevu.

Kupitia ubunifu wa kiteknolojia na kisayansi, kampuni moja ya humu nchini yenye hutengeneza rangi imeahidi kuondoa kero kwa wenye nyumba pamoja na wakazi kwa kubuni rangi itakayostahimili maji hayo.

Kampuni hiyo ya Dura Coat ilitangaza rangi hiyo almarufu AquaTech/ AquaArm Waterproofing Range, Jumanne katika mkutano uliowaleta pamoja wahandisi, kontrakta na wasambazaji wa rangi za Dura Coat, katika hoteli ya Villa Rosa Kempinski, Nairobi.

Rangi hiyo ambayo inapaswa kupakwa chini ya saa 8 na 12 baada ya mpaka-rangi kupaka mara ya kwanza, inanuiwa kutumika kwa ujuzi na wosia wa kontrakta ama mhandisi wa mjengo wowote.

Vile vile, kuna rangi tatu tofauti chini ya AquaTech/ AquaArm Waterproofing Range ambazo ni AquaTech PW 203, AquaTech LQ202 na AquaTech Bond Latex 503.

“AquaTech PW 203 na LQ202 zinaweza kutumika na gredi yoyote ya simiti,” akasema Meneja Mkuu wa kampuni ya Dura Coat Bw Aseem Doshi.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Bw Doshi pia alisema kuwa rangi hizo hukauka kwa saa 4-6 baada ya kupakwa na zinaweza kuwafaa watumiaji kwa miaka 10-15.

Hata hivyo, Sylvester Muli, mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wasanifu mijengo na Wapimaji ramani (BORAQS), alilalamikia kutokuwepo kwa vifaa na bidhaa zenye bei afueni ambazo hutumika kwenye ujenzi.

“Changamoto ya wapimaji ramani huwa kumudu bajeti ya miradi ya ujenzi huku wakiangazia bei kwenye soko,” akaongeza.

  • Tags

You can share this post!

Mvulana ashtakiwa kumtisha mama yake

Rais Kenyatta atia saini mswada tata wa vyama vya kisiasa

T L