Kampuni yazindua simu inayolenga wasanii

Kampuni yazindua simu inayolenga wasanii

NA WINNIE ONYANDO

KAMPUNI ya simu ya Tecno imezindua simu mpya inayolenga wasanii wa kutengeneza video za mtandaoni.

Simu hiyo Phantom X2 Series ina uwezo wa kunasa picha za ubora wa hali ya juu – sifa inayoifanya kuwa kivutio kwa watengenezaji wa video za mtandaoni.

Kwa mujibu wa meneja wa kampuni hiyo nchini, Anthony Brian Otieno, simu hiyo itawafaa sana wasanii wanaotengeneza video.

“Kampuni ya Tecno inanuia kuwaunganisha wengi kupitia bidhaa zake. Simu aina ya Phantom ni miongoni mwa bidhaa zitakazofanikisha uundaji wa video bora. Aidha, ni simu iliyo na uwezo mkubwa wa kuingia mtandaoni kwa haraka,” akasema Bw Otieno.

Akizungumza Jumatano baada ya uzinduzi huo, balozi wa Phantom X2 Eliud Kipchoge ambaye pia ni mwanariadha mashuhuri, alisema kwamba atatumia simu hiyo kunasa video akifanya mazoezi.

“Uzinduzi huu ni hatua muhimu. Itawafaidi wengi ulimwenguni,” akasema Bw Kipchoge.

Simu hiyo inapatikana katika maduka mbalimbali kwa malipo ya polepole.

  • Tags

You can share this post!

Ulanguzi wa watoto: Wafanyakazi 2 wa Mama Lucy wana kesi ya...

TUSIJE TUKASAHAU: NHIF ifanyiwe mageuzi iwahudumie Wakenya...

T L