Kampuni za mikate zaonywa dhidi ya kupotosha wateja kuhusu tarehe

Kampuni za mikate zaonywa dhidi ya kupotosha wateja kuhusu tarehe

Na Brian Ambani

MAMLAKA ya Kudhibiti Ushindani wa Kibiashara (CAK), imetoa ilani kwa viwanda vya kuoka mikate kwa kuweka habari za kupotosha kuhusu bidhaa zao.

Mamlaka hiyo ilisema uchunguzi umeonyesha kuwa kampuni hizo haziweki tarehe na mwezi kwenye karatasi za kufungia mikate, huku wengine wakichapisha maelezo kwenye matuta ya kufungia ambapo hayawezi kusomeka.

“Mamlaka imewaonya wanaokiuka kanuni kuhusu Sheria ya Ushindani na viwango vingine vinavyohitajika,” ilisema CAK.

Wenye viwanda hao wamekosa kuonyesha uzito wa mikate yao na viungo vinavyotumika.

Wengine hudai mikate yao imeongezwa virutubishi lakini hawakufafanua viungo walivyotumia.

Mkurugenzi wa CAK, Wang’ombe Kariuki, alisema kuwa wamiliki viwanda hawastahili kuchagua sheria watakazofuata, na kwamba wateja wana haki ya kupata habari kamili na sahihi kuhusu bidhaa au huduma zinazouzwa sokoni.

“Kampuni hizo hazikuwa zikitoa tarehe na mwezi ambapo bidhaa hizo zilitengezwa kwenye karatasi za kufungia mikate kwa mtindo unaofaa huku wengine wakichapisha maelezo hayo kwenye matuta ya kufungua kinyume na sheria,”

“Baadhi ya kampuni hizo zilitoa maelezo ya mwezi husika katika tarehe ambapo mikate hiyo inatarajiwa kuwa imeharibika kufikia wakati huo,”ilisema.

You can share this post!

Yaibuka raia wa Amerika aliteswa kisha kuuawa

Uteuzi wa Kidato cha Kwanza waahirishwa