Habari Mseto

Kampuni zafadhili vita dhidi ya Covid-19

March 31st, 2020 1 min read

Na LAWRENCE ONGARO

KAMPUNI mbili zimejitolea kusaidia na kufadhili vita dhidi ya virusi vya corona kwa kutoa dawa ya kunawa mikono.

Gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro, alikuwa mstari wa mbele kupokea shehena ya zaidi ya katoni 50 za dawa hiyo kutoka kwa kampuni ya Pipeline Ltd.

Wakati huo huo, kampuni ya pombe ya Kenya Breweries Ltd (KBL), ilitoa Sh 50 milioni zitakazosaidia kutengeneza dawa hiyo.

Dkt Nyoro alipongeza juhudi za kampuni hizo mbili kwa kuwafaa wananchi ili kupambana na Covid-19.

“Tunashukuru kutokana na hatua iliyochukuliwa na kampuni hizo mbili , kwani wanawajali wananchi wakati wa shida ambayo imekumba ulimwengu nzima,” alisema Dkt Nyoro.

Dkt Nyoro alisema tayari wameaaaanzisha kampeini ya kunyunyiza dawa kwa soko zzote muhimu katika kaunti ya Kiambu.

Alitaja soko la Madaraka, Makongeni, Ruiru, Juja, na Githurai,huku akisema baada ya siku mbili zijazo soko hizo zitaendelea na shughuli zake.

“Ninatoa mwito kwa wachuuzi wa soko hizo wadumishe usafi na wahakikshe wanatengana kwa umbali ili wasikaribiane. Kila mmoja ni sharti afuate maagizo yote yaliyowekwa na serikali,” alisema gavana huyo.

Alisema kila sehemu kuna maji na sabuni ya kunawa mikono na kwa hivyo serikali inaendelea kukabiliana vilivyona homa ya Covid-19.

Wakati wa hafla hiyo gavana aliandamana na kamishna wa kaunti ya Kiambu, Bw Wilson Wanyanga ambaye alisema sanitizer iliyotolewa itasambazwa katika sehemu muhimu katika kauti ya Kiambu.

Baadhi ya maeneo aliyolenga ni vijijini, sokoni, vituo vya magari vituo vya Polisi, na hata hospitalini.

Alisema uchunguzi uliofanywa katika mashinani umebainisha ya kwamba wananchi wanafuata maagizo ya serikali kikamilifu ya kunawa mikono kila mara.

Meneja wa biashara wa kampuni ya Breweries George Onsogo, alisema watahakikisha baada ya sanitizer hizo kupatikana zitasambazzwa kote nchini kupitia kaunti tofauti ili kila mwanancghi aweze kufaidika.