Macho kwa Kamworor akivizia rekodi ya dunia ya Eliud Kipchoge mjini Valencia

Macho kwa Kamworor akivizia rekodi ya dunia ya Eliud Kipchoge mjini Valencia

Na GEOFFREY ANENE

REKODI ya mbio za kilomita 42 ya wanaume ya saa 2:01:39 itakuwa hatarini Jumapili wakati wa makala ya 41 ya Valencia Marathon nchini Uhispania yaliyovutia magwiji Geoffrey Kamworor na Lawrence Cherono.

Waandalizi wa mbio hizo wameweka tuzo ya Sh31.8 milioni kwa mtimkaji atakayevunja rekodi ya dunia ya bingwa wa Olimpiki Eliud Kipchoge iliyowekwa jijini Berlin, Ujerumani mwaka 2018.

Bingwa mara mbili wa New York Marathon Kamworor na mfalme wa Chicago na Boston Marathon, Cherono wako katika orodha ya wanaopigiwa upatu kutawala mbio hizo ambazo zimevutia washiriki 16, 000 wakiwemo Wahispani 9,000.

“Nina ndoto kubwa katika marathon na ninataka kukimbia kasi ya juu iwezekanavyo na kuvunja rekodi. Valencia Marathon inatupatia fursa hiyo nzuri na ninaamini mashindano yatakuwa ya kufana,” Kamworor alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.

Ushindani mkubwa unatarajiwa kutoka kwa Waethiopia Herpasa Negasa na Chalu Deso, Mtanzania Gabriel Geayna raia wa Norway, Sondre Moen. Wakenya BBornes Chepkirui na Nancy Jelagat wako katika orodha ya wakimbiaji wanaopigiwa upatu kung’ara katika kitengo cha kina dada.

Wakenya Evans Chebet na Peres Jepchirchir walizoa mataji ya 2020 kwa rekodi mpya ya Valencia Marathon ya saa 2:03:00 na 2:17:16, mtawalia.

You can share this post!

Mwanaharakati mashuhuri David Kimengere arejea nchini baada...

Jumwa na wengine 6 wataka kesi ya ufisadi dhidi yao...

T L