Kananu kuapishwa kumrithi Mike Sonko

Kananu kuapishwa kumrithi Mike Sonko

Na RICHARD MUNGUTI

NAIROBI itapata Gavana mpya baada ya Mahakama ya Rufaa kuamuru Naibu Gavana Anne Kananu aapishwe mara moja.

Wakiamuru Bi Kananu achukue hatamu za uongozi wa Kaunti ya Nairobi, majaji Wanjiru Karanja, Jamila Mohammed na Jessie Lesiit walisema suala la kuapishwa kwake halikulalamikiwa katika mahakama kuu na mwanaharakati Okiya Omtata.

Bi Kananu aliyekuwa ameteuliwa Naibu wa Gavana Mike Sonko alikabiliwa na changamoto pale Jaji Antony Mrima alipoamuru asitwae hatamu za uongozi.

Jaji Mrima alihoji uhalali wa Bw Sonko kumteua Bi Kananu.

Kuapishwa kwa Bi Kananu kulipingwa na majaji hao watatu wakisema, “suala la kuapishwa halikuwa mojawapo ya tetezi za rufaa hiyo”.

Bw Omtatah na Bw Sonko waliwasilisha kesi ya kupinga kuapishwa kwa Bi Kananu aliyekuwa ameajiriwa katika idara ya masuala dharura na pia sekta ya maji.

You can share this post!

UMBEA: Penzi lina ladha ya kipekee, utamu, uchachu, uchungu...

Matiang’i atangaza ataunga Raila 2022

T L