Kane kusalia nje kwa muda mrefu baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu dhidi ya Liverpool

Kane kusalia nje kwa muda mrefu baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu dhidi ya Liverpool

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, sasa atasalia mkekani kwa kipindi kirefu baada ya kupata jeraha baya la kifundo cha mguu wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) dhidi ya Liverpool.

Kane, 27, aliondolewa uwanjani katika kipindi cha pili baada ya kupata jeraha alipokabiliwa na nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson.

Awali, Kane ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, alikuwa ameumizwa na kiungo wa Liverpool, Thiago Alcantara aliyemchezea visivyo mwanzoni mwa kipindi cha kwanza.

Baada ya kuondolewa uwanjani, nafasi ya Kane ilitwaliwa na Erik Lamela.

“Jeraha la pili lilikuwa baya zaidi kuliko la kwanza. Alitatizika sana uwanjani na ikatulazimu kumwondoa baada ya muda,” akasema Mourinho.

Mnamo 2018-19, Kane alipata tena jeraha la kifundo cha mguu na akalazimika kusalia mkekani kwa muda mrefu na hivyo kukosa jumla ya michuano saba ya waajiri wake.

Alirejea uwanjani kwa muda mfupi baada ya kupona na kujipata tena akisalia nje kwa kipindi cha miezi minne kati ya Januari na Aprili 2019 ambapo alikosa kuchezea Spurs katika jumla ya mechi tisa.

Nyota huyo aliumia kifundo cha mguu wa kulia mnamo 2017-18 na akakosa kuchezeshwa kwa mwezi mzima baada ya jeraha jingine la awali katika msimu wa 2016-17 kumweka nje kwa majuma manne ambapo alikosa mechi sita za Spurs.

You can share this post!

EPL: Liverpool wajifufua ugenini wakipiga tena Tottenham...

Raila ataka serikali ilegeze masharti ya ibada