Karua atoa ahadi ya kuzidi kutetea wanawake wote

Karua atoa ahadi ya kuzidi kutetea wanawake wote

NA KENYA NEWS AGENCY

MGOMBEAJI mwenza katika muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya; Bi Martha Karua amesema uteuzi wake umewashaajisha wanawake kuwania vyeo vya uongozi na akifaulu kushinda urais pamoja na Bw Raila Odinga, maslahi ya wanawake yatashughulikiwa.

Bi Karua aliwataka wanawake wampigie kura Bw Odinga akisema kuwa pamoja na kigogo huyo wa ODM wana rekodi ya kuchapa kazi na kupigania mageuzi nchini.

Alikuwa akizungumza katika Chuo Kikuu cha Garissa wakati wa maadhmisho ya miaka 70 ya Chama cha Maendeleo ya Wanawake ambapo aliwarai wawaniaji mbalimbali waendeleze kampeni za amani.

  • Tags

You can share this post!

Moto waangamiza watoto 10 wachanga hospitalini Senegal

Wakazi waulizia aliko gavana wao

T L