Makala

KASHESHE: Akanyagia stori kijanja

January 3rd, 2020 1 min read

Na THOMAS MATIKO

KICHUNA mwigizaji maarufu kule Bongo, Wema Sepetu kafunguka kuhusiana na taarifa kwamba mpenzi wake mpya kwa jina Danzak kamchumbia na sasa mipango ya ndoa ndio inaiva.

Hata hivyo mrembo huyo ambaye aliwatamanishia wengi mapenzi kipindi alichowahi kutoka na Diamond Platnumz, kaamua kukanyagia stori hiyo kijanja.

“Unajua siku zote jambo la kheri linaenda na kheri hivyo basi kama ikifika hiyo siku, mimi nitashukuru. Kikubwa ni kuomba hiyo siku ifike na jambo hilo litimie,” Wema kakanyagia.

Mrembo huyo ambaye kaishi maisha ya skendo na drama, kajitahidi sana kuishi maisha ya ukimya toka Julai mwaka huu baada ya kuhangaishwa sana na kesi ya kuvujisha video yake ya ngono.

Kesi hiyo ilimhangaisha mahakamani kwa miezi kadhaa kabla ya kutemwa baada ya kiongozi wa mashtaka kushindwa kuwasilisha mashahidi dhidi ya mrembo huyo. Toka wakati huo, amekuwa akicheza chini akihakikisha jina lake linaepuka kugonga vichwa vya habari.