KASHESHE: Amber Lulu apata sapoti

KASHESHE: Amber Lulu apata sapoti

NA SINDA MATIKO

MASTAA wa burudani Tanzania wameungana kumsaidia ex wake rapa CMB Prezzo, msupa mwanamuziki Amber Lulu.

Juzi kati Amber Lulu alifichua kwamba anapitia kipigo kila kukicha kutoka kwa mpenzi wake aliyezaa naye.

Amber alifichua manyanyaso ya kiukatili ambayo anapitia na mpenzi wake wa sasa ikiwemo kutishiwa kifo.

Baadhi ya picha alizoposti zilionyesha akiwa amepigwa mishono ya kutosha kutokana na majeraha ya kupigwa.

Sasa mastaa wa Bongo wakiongozwa na Shetta wameungana kumsapoti Amber huku wakisisitiza kuwa wanataka sheria ichukue mkondo.

“Nimemtafuta Amber na nimezungumza naye hali yake sio nzuri. Nimemshauri cha kufanya lakini pia nimezungumza na wenzangu kwenye Shirika letu la Sawa Tanzania kuona jinsi gani tunamsaidia,” Shetta amesema.

Kando na Shetta wengine waliojitokeza ni waigizaji wa kike.

Amber aliwahi kuwa na mahusiano na Prezzo na hata wakati mmoja kudaiwa kukaribia kufunga ndoa.

  • Tags

You can share this post!

KIPWANI: Hawa Nadra wan’leta ile vibe ya ‘Tatuu’

Rais kukopa kitita cha pesa kwa siku

T L