Makala

KASHESHE: Amtolea povu Ex wake

August 14th, 2020 1 min read

Na THOMAS MATIKO

NYOTA wa Bongo Flava Harmonize ameamua kumchomea picha demu wake wa zamani mwigizaji Jacqueline Wolper kufuatia madai ya msupa huyo kuwa jamaa alimwacha baada ya kupata sponsa mlami Sarah.

Baada ya kutemana na Wolper, Harmonize amekuwa kwenye mapenzi na Sarah ambaye walioana mwaka jana na kwa sasa ana ujauzito.

Imekuwa ikidaiwa kuwa Harmonize kadumu na Sarah kwa sababu mzungu huyo ana mkwanja mrefu kinoma na ndiye amekuwa akimpiga jeki pakubwa.

Lakini baada ya Wolper kumchokonoa, Harmonize kaamua kumtolea mabaya kwa kusema alimtema baada ya kutaka kutoka kimapenzi na bosi wake wa zamani Diamond Platnumz.

“Sio vizuri kuwasema wanawake lakini inaniumiza maana niliamua kukaa kimya lakini anavyozidi kufanya ‘interviews’, anasema mimi nilipata mzungu sponsa nikamwacha. Kilichotufanya tuachane ni hiki. Tulikuwa nyumbani kwa kaka yangu, bosi wangu wa zamani Diamond Platnumz tukawa tunaparty na bila haya, bila aibu akawa anamtaka Diamond kimapenzi,” Harmonize kafunguka hivi majuzi na blogu moja ya kule Bongo.

Harmonize anasema Wolper alijaribu kumtongoza sana Diamond ikiwemo kumuahidi kumzalia mtoto huku akidai kwamba alikuwa naye tu ili aweze kumfikia Chibu.

Stori hiyo Harmonize anasema Diamond alimwambia siku moja alipokuwa kalewa.