Makala

KASHESHE: Atema mkwara mzito

September 27th, 2019 1 min read

Na THOMAS MATIKO

MWIGIZAJI wa Bongo Movie, Wema Sepetu hana mpango wa kuolewa baada ya kutimiza umri wa miaka 30.

Wema ambaye amekuwa kwenye showbiz kwa miaka mingi anahoji kuwa kama hakupata mwanamume wa kumwoa miaka ya nyuma, haoni ni kwa nini aolewe sasa umri ukiwa umesonga.

“Sio siri nimeshaghairi kabisa suala la kuolewa kwa sasa. Kama hiyo bahati haikuwepo huko nyuma, basi imeshapita maana mchongo wa kufunga ndoa sasa hivi ni kurudishana nyuma tu bila sababu za msingi,” Wema kafunguka.

Kikubwa kwake kwa sasa ni suala la ni vipi ataweza kupata mtoto baada ya madaktari wake kumwelezea kuwa anaweza kushika ujauzito kuanzia mwakani baada ya kumaliza tiba ya kufungua mirija yake ya uzazi iliyokuwa imemgandia kwa zaidi ya miaka minane ambayo amekuwa akihangaika bila mafanikio.