KASHESHE: Azimio la Muhando

KASHESHE: Azimio la Muhando

NA SINDA MATIKO

WIKI mbili zilizopita Rose Muhando alitrendi Kenya na kwao Bongo baada ya kudai kuwa yupo sokoni akisaka mume mzungu.

Wengi waliamua kumchamba kwa kauli hiyo huku wengine wakitania kuwa kachoka ile mbaya.

Wapo wengine walibaki kumshangaa kwa kuwa ni msanii wa injili.

Lakini kama walidhani atahaha, basi anataka wafahamu kuwa hatishiki na kweli yupo kwenye mchakato wake wa kusaka mzungu.

Sasa ametetea kauli yake hiyo ya awali kwa kuongeza utamu akisema kuwa hataki tu mzungu yeyote ila anamtaka yule aliyekafunga.

“Ndoa ni kujaliwa sababu sio kitu cha kwenda kutafuta shambani. Mimi siwezi kumtafuta mwanamume, huo ni umalaya. Basi nitamwomba Mungu anipe mume na mimi nimechagua mzungu. Lakini sijaomba mzungu ngozi, nimeomba anipe mzungu mwenye hela niende nikahubiri injili. Mzungu ngozi ni hasara. Naamini sijavunja amri yoyote katika hili,” katupia.

You can share this post!

KASHESHE: ‘Mnikome!’

Sapit: Msiwachague wasiotekeleza ahadi

T L