KASHESHE: Bien atetea ‘wivu’ wa mkewe

KASHESHE: Bien atetea ‘wivu’ wa mkewe

NA SINDA MATIKO

BIEN-Aime Baraza kamkingia mke wake dansa Chiki Kuruka kuhusiana na kisanga cha wikendi iliyopita.

Staa huyo alikuwa akijiandaa kutumbuiza kwenye shoo ya Gin jijini Nairobi Jumamosi iliyopita.

Akiwa pembeni mwa steji kabla ya kupanda kwenye jukwaa rasmi, alitokea shabiki ambaye alionekana akimnengulia kiuno Bien.

Kilichofuata ni Chiki kumbumburusha dada yule na kisha kuwaita mabaunsa kuweka ulinzi.

Video baada ya kutrendi huku wengi wakidai Chiki ana wivu, Bien kamkingia.

“Jamani Chiki alikuwa anafanya kazi yake tu. Yule ni meneja wangu kwa hiyo alitaka kuhakikisha usalama wangu jukwani. Tukio lile na alichofanya Chiki, vilihusu kazi zaidi na wala sio masuala ya yeye kuwa mke wangu,” Bien Kamkingia.

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Kinaya Kenya kupatanisha mataifa mengine...

DOMO: Mtu asiniambie kuhusu mapenzi

T L