KASHESHE: ‘Chibu’ huyoo…azidi kupepea

KASHESHE: ‘Chibu’ huyoo…azidi kupepea

NA SINDA MATIKO

BAADA ya EP yake ya First of All, staa Diamond Platnumz ameanza maandalizi ya albamu yake itakayoandaliwa na produsa nguli wa Marekani, Swizz Beats.

Diamond kafichua hayo kwenye mahojiano ya podcast ya Afrobeats inayoongozwa na Adesope.

“Kila mtu anajua jinsi Swizz Beats alivyo mkubwa. Ningependa kumshukuru sana Swizz Beats kwa jitihada zake za kusukuma muziki wa Afrika kufikia kila eneo la dunia. Ni uamuzi mkubwa yeye kuamua kusukuma muziki wa Afrika, inaonyesha jinsi gani anavyotupenda. Kila mara nikienda Marekani huwa nashinda naye mara nyingi akinipa mawaidha ya muziki nini cha kufanya. Ni uamuzi wake wa kuandaa albamu yangu ya nne. Ndiye atakayekuwa produsa mkuu wa albamu hiyo,” Diamond amefunguka.

Hii ni hatua kubwa kwa Diamond kuweza kuandaliwa kazi na mume wa staa Alicia Keys, ambaye anaheshimika kwenye ulimwengu wa muziki Marekani akiwa amendaa kazi ya mastaa kibao kama vile Jay Z, Beyonce, Rick Ross, Lil Wayne, Kanye West miongoni mwa wengine.

Diamond alipata mafanikio makubwa na albamu yake ya A Boy From Tandale na anategemea mkono wa Swizz Beats utamzidishia mafanikio hata zaidi.

  • Tags

You can share this post!

KIPWANI: Toto la Kitaita lateka anga ya uigizaji

Wakazi wa Lamu wataka ahadi za Kibaki kwao zitimizwe

T L