KASHESHE: Eti mtasubiri ndoa sana!

KASHESHE: Eti mtasubiri ndoa sana!

NA SINDA MATIKO

SASA kama mlikuwa mnasubiria ndoa yake, basi mtasubiri sana sababu fisi Diamond Platnumz hana mpango wa kuoa hivi karibuni.

Diamond kadai ndoa imewapoteza wanamuziki wengi mastaa na yeye hataki mkosi huo umkute.Kwa maana hiyo ataendelea kuwachezea mademu jinsi afanyavyo huku akiendelea kuachia muziki.

“Suala la mimi kuoa sio sasa. Kama kutulia nimetulia ila sio kutulia kwa kuoa. Nimeona mastaa wakipotea baada ya kuoa na mimi nataka niendelee kutoa muziki mwingi, muziki mzuri. Mke anaweza akawa kikwazo kwenye kasi yako ya kuachia muziki mzuri, hili nimelishuhudia kutoka kwa marafiki wa karibu. Kwa maana hiyo, sio leo. Nitaoa nitakapokaribia kustaafu muziki,” kafunguka.

Kumbuka Diamond kwenye shoo ya Young African, Rich & Famous, alikiri wazi kwamba yeye ni ‘player’ (fisi) na hawezi kuwa mwaminifu kwa mwanamke mmoja.

Kwa maana hiyo, Zuchu ajipange kulilia chooni jamaa atakapomchoka.

  • Tags

You can share this post!

KIKOLEZO: Bazenga P Diddy

Eric Johana Omondi ajiunga na klabu ya soka ya Muangthong...

T L