KASHESHE: Ezekiel Mutua arudisha ngori

KASHESHE: Ezekiel Mutua arudisha ngori

NA SINDA MATIKO

KUFUATIA kurejeshwa kwa leseni za muziki, sasa wahudumu wa matatu na waandalizi wa shoo wapo kwenye ngori ya kupigwa faini ya hadi Sh500,000

Afisa Mkuu Mtendaji mpya wa MCSK, chama cha ukusayaji na ugavi wa mirabaha kwa wasanii, Ezekiel Mutua, amerejesha sheria hiyo ya utoaji wa leseni za muziki, kwa watumizi wa muziki kwenye kupromoti biashara zao.

Sheria hiyo ilisitishwa 2020 kufuatia kuzuka kwa janga la Covid-19.

Lakini sasa baada ya mambo kuanza kurudi kwenye mstari, Mutua anasema MCSK imeamua kurejesha utoaji wa leseni hizo ili waweze kuwakusanyia wanachama wao fedha za kutosha.

Kwa kwaida baadhi ya wadau huepuka kuchukua leseni hizi au kwenda kinyume. Hiyo sasa itakuwa ngori kufuatia kurejeshwa kwa seria hiyo.Kwa mujibu wa Sheria za Haki Miliki 2021 ibara ya 38 kipengele cha 2 na 7, ukiukaji wa kanuni hizi unaweza kukurusha jela.

“Mtu yeyote atakayetumia muziki au kazi ya fasihi hadharani bila ya kuwa na ruhusa ya mmiliki wa kazi hiyo atakuwa amevunja sheria za haki miliki,” kipengele cha 2 kinaeleza.

Kwa kosa hilo, “Mtu yeyote atakayepatikana na kosa la kwenda kinyume na kipengele cha 2, atatozwa faini isiyozidi Sh500,000 au hukumu ya kifungo kisichozidi miaka minne jela, au adhabu zote,” Kipengele cha 7 kinaeleza.

Hii ina maana kuwa hata wamiliki wa saluni, baa, na benki wapo kwenye hatari hii.

You can share this post!

DOMO: Sista-du Avril, usanii ni kujitolea

Rangers wadengua RB Leipzig na kufuzu kwa fainali ya Europa...

T L