KASHESHE: Hacheki na mtu!

KASHESHE: Hacheki na mtu!

NA SINDA MATIKO

SASA ni hatia kutumia maneno Freshi Barida kutangaza biashara yoyote ile pasi na idhini ya msanii Stivo Simple Boy.

Baada ya kauli hiyo kupata umaarufu, Stivo aliyebuni, amesajilisha kuwa hakimiliki.

Kwa maana hiyo, huwezi kutumia maneno hayo kupromoti aina yoyote ya biashara bila ya baraka zake.

“Freshi Barida ni hakimiliki ya Simple Boy. Huwezi kutumia kibiashara bila idhini yake. Itakuwa ni ukiukaji wa sheria,” menejimenti yake imetoa taarifa.

Tayari ameanza mchakato wa kuitumia kwa kuwekeza kwenye brandi ya mavazi yake. Freshi Barida aidha ni wimbo wake mpya aliouchia zaidi ya wiki mbili zilizopita.

  • Tags

You can share this post!

Huwezi ukang’olewa huku ukawania kule, DPP Haji...

KASHESHE: Lupita kuja nyumbani

T L