KASHESHE: Hayawi hayawi huwa!

KASHESHE: Hayawi hayawi huwa!

NA SINDA MATIKO

RIHANNA au ukipenda Bad Gal Riri, ameamua kupanua utajiri wake kwa kuingiza bidhaa zake za vipodozi katika soka la Kenya.

Msupa huyo ametangaza kuwa ataingiza bidhaa zake za Fenty Beauty kwenye soko kuanzia Mei 27, 2022.

Uzinduzi wa Fenty Beauty Kenya, utashabihiana na uzinduzi sawia katika mataifa ya Botswana, Ghana, Namibia, Nigeria, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe.

“Nimekuwa nikisubiri kwa hamu kubwa hili litimie. Fenty Beauty na Fenty Skin Scare hatimaye tunaingia Afrika,” aliposti taarifa hizo.

Upanuzi wa himaya yake ya kibiashara utamhakikishia mpunga zaidi.

Tayari ndiye mwanamuziki wa kike tajiri duniani akiwa na thamani ya dola 1.7 bilioni.

Asilimia kubwa ya pato lake imetokana na mauzo ya bidhaa zake za urembo.

  • Tags

You can share this post!

KASHESHE: Lupita kuja nyumbani

KASHESHE: Sasa auza sigara

T L