KASHESHE: Lupita kuja nyumbani

KASHESHE: Lupita kuja nyumbani

NA SINDA MATIKO

BAADA ya kuikosa pati ya Met Gala 2022, staa wa Hollywood Lupita Nyong’o, anatarajiwa kuzuru nyumbani wikendi ijayo.

Lupita atakuwa miongoni mwa wageni wa heshima kwenye warsha ya Afri-Cities itakayofanyika Kisumu.

Babake, Profesa Anyang’ Nyong’o, atakuwa mwenyeji wa warsha hiyo itakayofunguliwa na Rais Uhuru Kenyatta Mei 17.

Lupita atahudhuria akiwa balozi wa kheri njema wa Afri-Cities ambalo ni kongamano la siku tano kujadili ustawi wa miji.

Tangu ageuke staa na kushinda tuzo za Oscars 2012, Lupita hajawahi kufanya mahojiano yoyote na wanahabari Wakenya.

Safari zake nchini zimekuwa za kimya kimya akihakikisha anawaepuka wanahabari.

You can share this post!

KASHESHE: Hacheki na mtu!

KASHESHE: Hayawi hayawi huwa!

T L