KASHESHE: ‘Nameless alinichanua’

KASHESHE: ‘Nameless alinichanua’

NA SINDA MATIKO

MAUREEN Kunga amefichua namna Nameless alivyomshauri baada ya kutapeliwa na produsa aliyekuwa akimfanyia kazi nguli huyo.

Kunga anayeunda kundi la Elani, anasema kipindi anaanza muziki akiwa hajulikani, alikuwa kwenye studio moja ambayo Nameless alikuja kurekodi.Wakati Nameless anarekodi ngoma, lejendari huyo aliomba kufanyiwa voko na kuendana na wimbo wake. Hapo produsa akamwambia amwachie hiyo.

“Produsa akaniomba kama ninaweza kufanya voko nikakubali sababu ndio kazi niliyoanza nayo kabla ya kuja kuwa mwanamuziki wa kujitegemea.”

Baadaye Maureen alikuja kugundua kuwa Nameless alimlipa produsa hela ya utengenezaji wa voko hizo ila yeye hakupata kitu.

“Nilipokutana na Nameless baadaye na kumwelezea kwamba sikulipwa chochote licha ya yeye kumlipa produsa, alichoniambia ni kwamba, nahitaji kuwa makini sana hasa na watu wanaotabasamu usoni mwangu. Sijawahi kusahau ushauri huo.”

Kwa sasa msupa amejitosa kwenye masuala ya uigizaji baada ya Elani kuamua kila mmoja afanye miradi ya kibinafsi.

  • Tags

You can share this post!

Mtoto Asome: Wanafunzi 50 kujiunga na shule baada ya...

Leliman ahukumiwa kunyongwa kwa mauaji ya wakili Willie...

T L