KASHESHE: Nay aachilia ‘vawulence’

KASHESHE: Nay aachilia ‘vawulence’

NA SINDA MATIKO

RAPA asiyepima maneno Nay Wa Mitego amewatolea uvivu wasanii wa muziki wa Bongo ambao wamefanya tabia za kutoka kimapenzi na wanawake wenye pesa.

Nay anasema tabia hizo za kuwekwa na wanawake wenye pesa ni hatari sana kwani ni rahisi mtu kujisahau.

“Wasanii wakipata wanawake wenye hela wanasahau kazi iliyowafanya wapendwe. Wanakuwa wapo bize sana na mapenzi wakiachwa ndio wanakumbuka kurudi kazi na mambo yanakuwa magumu kuanza upya,” Nay kakemea.

Kulingana naye, mashabiki wa siku hizi wanasahau haraka kutokana na wasanii kuwa wengi tena wakali hivyo mtu anapojipoteza anasahaulika na kurudi kuiteka ile hadhira inakuwa mtihani.

  • Tags

You can share this post!

Rais kukopa kitita cha pesa kwa siku

Mauaji ya wajane Lugari yaibua hasira

T L