KASHESHE: ‘Nimekoma’

KASHESHE: ‘Nimekoma’

NA SINDA MATIKO

MTANGAZAJI wa zamani wa runinga Betty Kyallo, hana mpango wa kumwanika tena mpenzi wake hadharani akitaja hilo kuwa kosa kubwa.

Betty amekuwa na desturi ya kuitangazia dunia kila anapokuwa kwenye penzi, ila sasa anasema amejishika sikio.

“Nimefanya makosa mengi kwenye maisha yangu ya kimahusiano. Na ingawaje sijutii yaliyotokea katika maisha yangu, sifikiri nitawahi tena kumwanika mpenzi wangu sababu kwa kufanya hivyo, nimegundua ninajiletea presha kibao,” kasema.

Ameapa kumficha mpenzi wake akisisitiza kuwa hatua hiyo itamsaidia sana sio tu kumwelewa mwenzake lakini pia kudumisha penzi.

  • Tags

You can share this post!

Wajackoyah kutumia bangi, nyoka na mbwa kukwamua Kenya...

KIKOLEZO: Wueeh, kimemuumania!

T L