KASHESHE: Sasa auza sigara

KASHESHE: Sasa auza sigara

NA SINDA MATIKO

WIKI moja tu baada ya kuzengua Kenya, mzee wa vishasha sasa ameamua kuja na jipya.

Harmonize ametangaza mchakato wa kuja na brandi yake ya sigara ‘Tembo’.

Staa huyo anasema tayari ameanza kumsaka mdhamini ambaye watashirikiana naye kwenye ukarabati wa brandi hiyo kabla ya kuizindua rasmi.

Msanii huyo anasema lengo lake ni kuwawezesha wakulima wa tumbaku Tanzania.

“Sio lazima mpaka waingie Wachina, sisi wenyewe tunaweza. tumbaku bora kabisa inalimwa Tanzania,” kasema.

Harmonize ambaye ni mraibu mkubwa wa kufukisha moshi, amewahi kuwa balozi wa sigara aina ya Yes Cigarrette inayoundwa na kampuni ya Mastermind Tobacco Limited.

  • Tags

You can share this post!

KASHESHE: Hayawi hayawi huwa!

KASHESHE: Wajigeuza mbogo!

T L