KASHESHE: ‘Siri ya ndoa kunyenyekea’

KASHESHE: ‘Siri ya ndoa kunyenyekea’

Na PAULINE ONGAJI

NYOTA wa injili Mercy Masika kafichua siri moja ya kuhakikisha ndoa inadumu kwa muda mrefu ni pale mwanamke anapokuwa mnyenyekevu kwa mumewe.

Ni wazo wanalopinga wanawake wengi katika karne hii ya sasa.

Lakini machoni mwake Masika, ukosefu wa sifa hiyo ndio sababu ndoa nyingi zinabuma.

“Nilishtumiwa sana kwa kuwa mnyenyekevu kwa mume wangu nilipoolewa. Ila watu wanasahau kabisa maandiko yanasema kuwa unyenyekevu kwa mumeo ni heshima kwake. Unyenyekevu sio utumwa kama wengi wanavyofikiria. Ndio sababu ndoa yangu imefanikiwa,” kasema.

Mrembo huyo ambaye ni mama wa watoto wawili kadumu kwenye ndoa yake kwa miaka 13 sasa.

You can share this post!

Man-United wasitisha mazungumzo ya kurefusha mkataba wa...

Kune Food kutumia teknolojia kuwalisha Wakenya vyakula vya...

T L