KASHESHE: Wajigeuza mbogo!

KASHESHE: Wajigeuza mbogo!

NA SINDA MATIKO

DIAMOND Platnumz na Zuchu wamejigeuza mbogo kufuatia maelekezo ya Halmashauri ya Mawasiliano Tanzania – TCRA – kuwataka waukarabati upya wimbo wao wa ‘Mtasubiri’.

Wimbo huo uliokamata nafasi ya kwanza kwa wiki tatu toka ulipoachiwa, umedaiwa kuzua ukakasi na TCRA.

Kulingana na TCRA, wimbo huo haupaswi kupeperushwa kwenye chombo chochote cha habari Tanzania.

Amri hiyo ni hadi pale wasanii hao watakapofuta au kurekebisha kipande kidogo kinachomwonyesha Zuchu akiwa kanisani.

Hata hivyo Diamond na Zuchu wamejitia hamnazo na kukosa kufanya mabadiliko hayo siku nne baadaye.

Aidha wameikemea TCRA kwa kuwaonea wakisistiza kuwa hawakufanya kosa lolote.

  • Tags

You can share this post!

KASHESHE: Sasa auza sigara

Zetech Sparks yapania kumaliza tatu-bora KWPL

T L