KASHESHE: ‘Walinitilia sumu’

KASHESHE: ‘Walinitilia sumu’

NA SINDA MATIKO

HIVI unakumbuka kile kisanga cha Ommy Dimpoz kulazwa hospitalini akiwa hali mahututi miaka mitano iliyopita?

Dimpoz sasa kasema alitiliwa sumu.

“Walinitilia sumu lengo likiwa ni kuniua. Ilikuwa nusu nife nimfuate mamangu,” kawaambia mashabiki wakati akitumbuiza kwenye tamasha la Break Point.

Mwanamuziki huyo alipoteza sauti ghafla wakati akiwa kwenye sherehe fulani na kumpelekea kulazwa kwa miaka miwili.

Sauti yake ilipotea kabisa na alilazimika kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini na kisha Ujerumani ili kurekebisha mambo.

Sehemu kubwa ya gharama ya matibabu yake iliyozidi Sh6 milioni, ilitolewa na Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho.

You can share this post!

Michezo ya Jumuiya ya Madola: McGrath asema Shujaa imeiva...

LISHE: Faida za maziwa ya ngamia

T L