NA SINDA MATIKO
MWANAMUZIKI wa lebo ya WCB Zuhura Othman almaarufu Zuchu kamtaka mumewe asiwe na matarajio makubwa sana juu yake hasa kuhusu mwonekano wake.
Zuchu baada ya kuusoma upepo, amemtaka mwanamume atakayeishia kutaka kumwoa kuridhika na mwonekano wake hasa makalio yake madogo.
“Mpendwa mume wangu mtarajiwa, najua huko ulipo una matarajio makubwa sana juu ya mwonekano wangu ila naomba nikuondolee tarajio moja, sina ta** mpenzi.” Zuchu aliandika kwenye Snapchat.
Wapo wale wanaohisi maelezo yale aliyalenga kwa bosi wake Diamond Platnumz ambaye amehusishwa naye kwa muda.