Kasisi akamatwa kuhusiana na wizi wa simu Kirinyaga

Kasisi akamatwa kuhusiana na wizi wa simu Kirinyaga

Na GEORGE MUNENE

KASISI wa kanisa la Angilikana jana Ijumaa alikamatwa na polisi katika Kaunti ya Kirinyaga, kwa kushukiwa kuiba simu.

Kasisi huyo alikamatwa eneo la Kagio na kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kianyaga, eneobunge la Gichugu.

Kulingana na Mkuu wa Polisi Kirinyaga Mashariki, Bw Anthony Wanjuu, kasisi huyo aliyetawazwa hivi majuzi, alikuwa anasubiri kutumwa kuhudumu katika parokia yoyote eneo hilo.

Bw Wanjuu alisema mshukiwa anazuiliwa kwa wizi wa simu ya mmoja wa viongozi wa kanisa hilo.

Ilielezwa kuwa mshukiwa alikuwa amepatiwa lifti na kiongozi huyo alipodaiwa kutoa simu mfukoni mwake na kuificha.

Baadaye kasisi aliposhuka kutoka kwa gari hilo, mhubiri huyo aligundua simu yake ilikuwa imetoweka na akaripoti kwa polisi.

“Tulipopokea habari kuhusu wizi wa simu tulianza kufanya uchunguzi uliobainisha kuwa kasisi alikuwa na simu iliyoibwa na tukamkamata ili kumhoji,” akaeleza.

You can share this post!

Wanajeshi 4 wa Tanzania wajeruhiwa

TUSIJE TUKASAHAU

T L